BBC navigation

Washukiwa wataka kesi ICC kuakhirishwa

Imebadilishwa: 14 Februari, 2013 - Saa 15:46 GMT

Uhuru Kenyatta na mshukiwa mwenzake ambaye pia ni mgombea mwenza William Ruto

Mgombea wa urais nchini Kenya Uhuru Kenyatta na aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura , wameitaka mahakama ya ICC kuakhirisha kesi yake ili kuwaruhusu wajiandae.

Ombi hili limetolewa na mawakili wa Kenyatta na Muthaura wakisema kuwa upande wa mashtaka ulichelewesha ushahidi wake na hivyo hawakuwa na muda wa kutosha kujiandaa.

Mawakili wa wawili hao, Kari Khana na Stevenes Kay , walilalamika wakisema upande wa mashtaka unabadili mfumo wa kesi hizo.

Kenyatta, ambaye alikuwa waziri wa fedha alishtakiwa kwa kuwa mmoja wa wahusika wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 ambapo zaidi ya watu 1,200 waliuawa na maelfu ya wegine kuachwa bila makao.

Kufuatia ombi la mawakili hao la kuakhirishwa kwa kesi hiyo,wadadisi wanasema huenda ikamfaa Uhuru hasa baada ya uchaguzi mkuu tarahe nne mwezi Machi,

Wakiongea katika kikao mjini Hague, walisema kuwa, kudumaa kwa shughuli za ICC , viongozi wa mashtaka waliwaacha na ufahamu mdogo sana kuhusu kesi inayomkabili Uhuru na washukiwa wenzake.

"tunataka mashtaka haya kuchunguzwa vyema, '' alisema wakili wa Uhuru, Steven Kay, ambaye alisema hata hajapata muda wa kupitia ushahidi uliotolewa.

Kenyatta, ambaye alifuatilia kikao hicho kwa video akiwa nchini Kenya, alisema mara moja tu kuwa alielewa bado anaweza kutakiwa kufika Hague na majaji wa kesi hiyo.

Wawili hao pamoja na washukiwa wengine watatu, akiwemo mgombea mwenza wa Uhuru , william Ruto wanakabiliwa na kosa la kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Mawakili hao pia walikosoa upande wa mashtaka na kusema kuwa walikubali kutumia mashahidi waliotoa ushahidi wa uongo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.