Jaribio la 3 la Nuklia Korea Kaskazini

  • 12 Februari 2013
Jaribio la Bomu la nuklia nchini Korea Kaskazini

Korea kaskazini imetekelezea jaribio la tatu la silaha zake za Nyuklia.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema kuwa jaribio hilo limetekelezwa kwa njia salama na kwamba wanasayansi walilipua bomu dogo la atomiki ambalo lilikuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko mabomu yaliyofanyiwa majaribio katika siku za nyuma.

Waandishi wanasema mlipuko huo wa chini ya ardhi huenda ukaipa Korea kaskazini uwezo wa kujenga silaha ya nyuklia ilio na udogo wa kutumika kwenye kombora la masafa marefu.

Rais Obama ametaja hatua hiyo kama kitendo cha uchokozi mkubwa kinachokiuka uwajibikaji wa nchi hiyo wa maazimio ya Umoja wa mataifa.

Wakati huohuo China ambayo ni mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini imepinga vikali jaribio hilo la nyuklia.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje imesema China inaunga mkono amani na utulivu katika rasi ya Korea.