Ghasia zaidi nchini Misri

Imebadilishwa: 21 Disemba, 2012 - Saa 12:58 GMT
Raia wa Misri wakiandamana

Raia wa Misri wakiandamana

Kumekuwa na makabiliano kati ya Waislamu wenye itikadi kali na wapinzani wao mbele ya msikiti mkubwa zaidi Mjini Alexandria nchini Misri, katika mkesha wa raundi ya pili ya kura ya maoni yenye utata kuhusu katiba mpya.

Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi kuyatawanya makundi hayo mawili nje ya msikiti huo wa Al-Qaed Ibrahim, ambao pia ulikuwa ukumbi wa machafuko mabaya siku ya Ijumaa iliyopita.

Katiba hiyo imetajwa kama inayowapendelea Waislamu wenye itikadi kali lakini wanasiasa wasiogemea upande wowote na Wakristu wamepinga vikali katiba hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.