Mfungwa wa kisiasa afa gerezani Tunisia

Imebadilishwa: 17 Novemba, 2012 - Saa 15:51 GMT


Nchini Tunisia mfungwa mmoja wa kisiasa, aliyekuwa akisusia chakula tangu alipokamatwa kwa kushambuliia ubalozi wa Marekani mwezi Septemba, amefariki.

Waandamanaji waliwasha moto ubalozi wa Marekani mjini Tunis, mwezi Septemba

Muhammed Bakhti alikuwa mfuasi wa kundi la dini ya Kiislamu.

Bwana Bakhti ni mfungwa wa pili kufariki juma hili kwa sababu ya kususia chakula.

Wafungwa kadha wa madhehebu ya Salafi, wenye mrengo mkali wa Kiislamu, wamegomea chakula kulalamika juu ya hali ya magereza.

Mwezi Septemba, polisi waliwakamata watu zaidi ya 100 baada ya kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Tunis, kwa sababu walikerwa na video iliyokejeli Uislamu iliyotengenezwa Marekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.