BBC navigation

ICC : Waafrika waonyeshe ushujaa

Imebadilishwa: 24 Mei, 2012 - Saa 04:24 GMT

Mwendesha mashtaka mkuu mpya katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Fatou Bensouda, amesema wababe wa kivita wanawatisha viongozi wanaojaribu kuwatia mbaroni.

Bi Bensouda ametoa wito kwa viongozi wa Afrika wasikubali kutishwa na viongozi kama vile jenerali muasi Bosco Ntaganda.

Bosco Ntaganda

wababe wanawatisha viongozi Afrika

Jenerali Ntaganda anakabiliwa na tuhuma za uhalifu wa kivita na kwa kuwasajili watoto vitani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akizungumza na BBC, Bi Bensouda amesema kuwa wababe hao wanawatisha viongozi kuwa ikiwa hawata legeza kasi ya kuwasaka basi wataendelea kuwaua watu.

Katika siku za hivi karibuni, mamia ya watu wameuawa huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wanajeshi wanamsaka Jenerali Ntaganda.

Mwezi March mwaka huu, mahakama ya ICC ilimpata mshirika wake mkuu wa Jenerali Ntaganda, Thomas Lubanga na hatia ya kutekeleza uhalifu wa kivita mashariki mwa Congo.

Bi Bensouda ambaye ni wakili kutoka Gambia ni mwaafrika wa kwanza kuteuliwa kama mwendesha mashtaka katika mahakama hiyo.

Ataanza kutekeleza majukumu yake mwezi ujao baada ya kustaafu kwa Louis Moreno Ocampo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.