Kanisa lashambuliwa mjini Khartoum

Imebadilishwa: 22 Aprili, 2012 - Saa 17:28 GMT

Kanisa moja mjini Khartoum, Sudan, limechomwa moto na Waislamu.

Rais al_bashir akizungumza kwenye mkutano wa chama chake mjini Khartoum

Taarifa zinasema watu mia kadha waliandamana jana usiku hadi kwenye kanisa, ambalo linatumiwa na Wakristo kutoka Sudan Kusini.

Hakuna ripoti za mtu kujeruhiwa.

Sudan Kusini, ambayo watu wake wengi ni Wakristo au wafuasi wa dini za kijadi, ilipata uhuru Julai mwaka jana.

Lakini nchi mbili hizo zimeshindwa kutatua mizozo yao kuhusu visima vya mafuta na mipaka.

Mapigano yamezidi hivi karibuni katika maeneo ya mpakani, huku kuna wasiwasi kuwa vita kamili vitazuka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.