Syria yafanya kura ya maoni

Imebadilishwa: 26 Februari, 2012 - Saa 10:04 GMT

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanywa nchini Syria hii leo, ingawa ghasia zinaendelea nchini.

Wanajeshi wa Syria wakipita biramu inayosema "katiba ya Syria"

Kura hiyo ni muhimu katika utaratibu wa kuleta mabadiliko yaliyopendekezwa na Rais Bashar al-Assad, ili kujibu maandamano dhidi ya serikali yake yaliyoanza karibu mwaka mzima uliopita.

Katiba mpya itaruhusu mfumo wa vyama vingi nchini Syria.

Upinzani umetoa wito watu waisusie kura hiyo.

Mwandishi wa BBC anasema haijulikani vipi kura ya maoni inaweza kufanywa kati ya mtafaruku ulioko nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.