bbc.co.uk navigation

Viongozi wa Somalia wakubaliana

Imebadilishwa: 18 Februari, 2012 - Saa 14:42 GMT

Viongozi wa Somalia wametia saini mkataba ambao wanataraji utamaliza msuko-suko wa nchi hiyo.

William Hague, waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Uingereza alipokuwa Somalia.

Inaazimiwa kuwa na bunge jipya litalokuwa na baraza la pili la wazee na serikali za majimbo.

Wanawake watakuwa asili-mia-30 ya wabunge.

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na serikali ya sasa, utawala wa majimbo mawili, na wanamgambo wanaounga mkono serikali, yatajadiliwa juma lijalo, kwenye mkutano wa London kuhusu Somalia.

Lakini kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambalo linadhibiti sehemu kubwa ya kati na kusini mwa nchi hiyo, hawakushiriki kwenye makubaliano hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.