BBC navigation

Brigedia-Jenerali auwawa Damascus

Imebadilishwa: 11 Februari, 2012 - Saa 13:26 GMT

Shirika la habari la taifa la Syria linasema kuwa watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa afisa wa daraja ya juu katika jeshi, kwenye mji mkuu, Damascus.

Jeshi la Syria

Inafikiriwa hayo ni mauji ya kwanza ya afisa wa jeshi mjini humo, tangu maandamano dhidi ya Rais Bashar al-Assad kuanza mwezi wa March, mwaka jana.

Shirika hilo limearifu kuwa watu watatu walimfyatulia risasi Brigadier-Jenerali Issa al-Khouli, alipotoka nyumbani kwake.

Taarifa iliwalaumu magaidi.

Hapo jana, watu kama 25 walikufa kwenye mashambulio ya mabomu, katika mji wa pili kwa ukubwa, mji wa Aleppo.

Na wanaharakati wanaopinga serikali ya Syria wanasema watu kama wane wameuwawa katika mji wa Homs, kwenye mashambulio mepya ya jeshi la serikali.

Wanasema mizinga imeshambulia tena mitaa ya upinzani mjini humo.

Waandishi wa habari wanasema raia hawawezi kujihami wala kuukimbia mji.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.