bbc.co.uk navigation

Syria: Watu wengi wauawa Homs

Imebadilishwa: 8 Februari, 2012 - Saa 12:10 GMT
Rais wa Syria Bashar al-Assad

Rais wa Syria Bashar al-Assad

Vikundi vya upinzani nchini Syria vinasema kwamba majeshi ya serikali yameushaumbulia mji wa Homs kwa makombora mengi, licha ya rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad kutoa ahadi ya kufanya mazungumzo na upinzani.

Mji huo wa Homs umekuwa ukishambuliwa kwa makombora kwa siku tano sasa; na majeshi ya serikali yanasemekana kukaribia maeneo yanayomilikiwa na vikundi vya upinzani.

Wanaharakati wanasema zaidi ya watu 40 wamefariki dunia kufuatia kurushwa kwa makombora lakini ni vigumu kubainisha jambo hili.

Mashambulio haya yanakuja siku moja baada ya Rais Bashar al-Assad kumhakikishia Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, huko Damascus kuwa mapigano yangesitishwa na mazungumzo kufanyika.

Urusi na China zilipiga kura ya turufu kupinga azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa wiki iliyopita.

Mwandishi wa BBC, Paul Wood, ambaye yuko nje ya mji wa Homs na wapiganaji waasi, anasema watu wa mji huo wanahofia mashambulio ya nchi kavu.

Mwandishi wa BBC mjini Beirut, Jim Muir, anasema idadi ya watu waliouawa huenda si ya uhakika kwa sababu inajumuisha watoto 18 ambao walikuwa wamezaliwa kabla ya wakati wao, na ambao walifariki dunia wakati umeme ulipokatika na mashine za kuwahifadhia kushindwa kufanya kazi.

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.