bbc.co.uk navigation

Boko Haram yakiri kufanya shambulio

Imebadilishwa: 9 Februari, 2012 - Saa 00:01 GMT
Mji wa Kaduna

Mji wa Kaduna

Wapiganaji wa Kiislam wa kundi lenye itikadi kali la Boko Haram wamekiri kwamba walifanya shambulio la kujilipua nje ya kambi ya jeshi katika jiji la Kaduna nchini Nigeria.

Mtu mmoja aliyevaa nguo za kijeshi alijilipua nje ya kambi hiyo ambayo ni mojawapo wa kambi ambazo zina ulinzi mkali nchini humo.

Msemaji wa kundi la Boko Haram pia amesema kwamba walijaribu kutekeleza shambulio lingine katika kambi ya askari wa anga.

Kundi hilo limesema linataka kupindua serikali ya Nigeria na badala yake kuhakikisha nchi hiyo inatawaliwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu.

Wanamgambo wa Kiislam wameua mamia ya watu kaskazini mwa Nigeria.

Mwandishi wa BBC, Abdullahi Kaura Abubaker, ambaye yuko kaskazini mwa Nigeria anasema kwamba kushambuliwa kwa mji wa Kaduna na kundi la Boko Haram ni tukio ambalo linaweza kuwa na athari kubwa katika siasa za Nigeria.

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.