Iran itaacha kuuza mafuta Ulaya

Imebadilishwa: 4 Februari, 2012 - Saa 16:39 GMT

Waziri wa mafuta wa Iran amekariri kuwa nchi yake itaacha kusafirisha mafuta kwa baadhi ya mataifa ya Ulaya, hata kabla ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya mafuta ya Iran kuanza kutekelezwa mwezi wa July.

Rostam Ghasemi, waziri wa mafuta wa Iran

Waziri Rostam Qasemi hakueleza nchi gani zitaathirika.

Alisema kutakuwa na mtafaruku katika masoko ya mafuta ya kimataifa, ikiwa mafuta ya Iran yatasusiwa.

Umoja wa Ulaya na Marekani hivi karibuni, ziliweka vikwazo vipya vikali dhidi ya Iran, wakiishutumu kuwa inatengeneza silaha za nuklia, kisirisiri.

Iran inasema mradi wake wa nuklia ni wa amani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.