bbc.co.uk navigation

Ghasia Senegal kupinga Wade kuania urais

Imebadilishwa: 28 Januari, 2012 - Saa 10:01 GMT

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amewasihi wananchi wawe watulivu baada ya maandamano ya ghasia kuzuka kufuatia uamuzi wa mahakama kumruhusu agombee muhula wa tatu wa urais.

Ghasia mjini Dakar, Senegal


Bwana Wade, mwenye umri wa miaka 85, alisema kuonesha hasira kwa fujo hakutaleta tija yoyote.

Alitokeza kwenye televisheni huku ghasia zinatapakaa katika miji kadha ya Senegal.

Katika mji mkuu, Dakar, vizuizi viliwekwa, magari yalipinduliwa na maduka kadha yalichomwa moto.

Wakuu wanasema askari polisi mmoja aliuwawa.

Mpinzani maarufu, mwimbaji Youssou N'Dour, ameonya kuwa hukumu ya mahakama ya katiba haitakubalika.

Mahakama hayo yalitupilia mbali ombi la Bwana N'Dour kutaka kugombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.