bbc.co.uk navigation

Wanigeria kwenye lenzi

Imebadilishwa: 22 Disemba, 2011 - Saa 20:34 GMT

Picha kutoka kwenye kitabu kilichoandikwa kwa heshima ya wapiga picha wa Nigeria kilichozinduliwa mjini Lagos na London

  • George Osodi, Ogoni Boy, 2007. Kutoka mfululizo wa picha Oil Rich Niger Delta
    Kitabu hiki kinaonyesha kazi za wasanii tisa, akiwemo George Osodi, mwandishi wa picha aliyoiita Ogoni Boy. Anaangazia athari za kibanadamu na kimazingira za uzalishaji wa mafuta usiokuwa na usimamizi
  • George Osodi, Tapioca Uzere, 2008. Kutoka mfululizo wa picha za Orange Light
    Picha hii nayo iliyopigwa na Bw Osodi, inaonyesha mchakato wa kutengeneza muhogo
  • Emeka Okereke, Long Wait, Paris 2005
    Picha imepigwa na Emeka Okereke ambapo iko katika gamba la kitabu cha Long Wait, Alipiga picha hii mjini Paris
  • Emeka Okereke, Suffering and Smiling 2, Lagos 2004
    Suffering and Smiling 2 nayo ilipigwa na Bw Okereke mjini Lagos mwaka 2004
  • Uche Okpa-Iroha, Untitled. Kutoka mfululizo wa picha za Underbridge Life
    Kazi iliyotokana na mfululizo wa picha zenye jina Underbridge Life zilizopigwa na Uche Okpa-Iroha, mwanaharakati wa afya ya figo ambaye baadae aliamua kuwa mpiga picha
  • Adolphus Opara, The Rush, 2008, kutoka sherehe za mwaka za uvuvi wa samaki za Argungu
    The Rush ilipigwa na Adolphus Opara mwaka 2008 wakati wa sherehe za mwaka za uvuvi wa samaki za Argungu kaskazini- magharibi mwa Nigeria.
  • Jide Alakija, Clean Shoes, 2008. Kutoka mfululizo wa picha za Page Boy
    Jide Alakija anayeishi mjini London anajulikana kwa picha zake za harusi.
  • Andrew Esiebo, Surviving Dreams
    Bi Atawodi, aliyeandaa kitabu hicho chenye picha kwa miaka minne, ameiambia BBC kuwa baadhi ya nakala hizo zitatolewa kama msaada kwenye maktaba na idara za utafiti. Picha hii, Surviving Dreams, imepigwa na Andrew Esiebo
  • Andrew Esiebo, Members Only, 3
    Bw Esiebo pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho Members Only
  • Amaize Ojeikere, Dr Know All. Katika mfululizo wa picha za The Market Place
    Picha hii, iliyopigwa na Amaize Ojeikere, inaitwa Dr Know All
  • Ty Bello. Kutoka mfululizo wa picha za Madam Ekundayo
    "Mama Ekundayo ni mwanamke niliyekutana naye mwaka 2003. Alikuwa na umri wa miaka 86 wakati huo na hakuwa na fedha hata hivyo amewatunza takriban watoto 400-500 katika maisha licha ya kutokuwa na uwezo." Alisema Bi Bello
  • Yetunde Ayeni-Babaeko, Untitled, 2009. Kutoka mfululizo wa Drei Dreiecke
    Kazi hii ambayo haijapewa jina imepigwa na Yetunde Ayeni-Babaeko, ambaye alisomea fani ya upigaji picha Ujerumani na ana kampuni ya matangazo mjini Lagos
  • Jide Alakija, No More Lies, 2008
    Picha hii nayo imepigwa na Jide Alakija
  • Ty Bello. Kutoka mfululizo wa picha za Femi
    Femi Kuti, mmoja wa watoto wa kiume mwanamuziki maarufu wa Nigeria Fela Kuti, iliyopigwa na kamera ya mwanamuziki mwenzake na mpiga picha Ty Bello

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.