8 Agosti, 2011 - Imetolewa 11:28 GMT

Kambi ya mateso yagunduliwa Zimbabwe

BBC Panorama imegundua kwamba, kambi ya mateso inayosimamiwa na majeshi ya usalama ya Zimbabwe inafanya shughuli zake katika eneo lenye utajiri wa almasi, Marange.

Kipindi hicho kilizungumza na walioathirika hivi karibuni wakielezea walivyopigwa sana na kudhalilishwa kijinsia.

Almasi ya Zimbabwe

Madai hayo yanatolewa huku Umoja wa Ulaya EU ukishinikiza kuruhusu baadhi ya almasi zilizopigwa marufuku kutoka nchi hiyo inayoongozwa na Rais Robert Mugabe kurejeshwa kwenye masoko ya dunia.

Serikali ya Zimbabwe haijasema lolote kuhusu utafiti huo wa BBC.

Katika nyaraka iliyoonekana na BBC, EU ulisema kuwa sasa una imani kuwa migodo miwili eneo hilo zinafikia viwango vya kimataifa na kutaka almasi zinazoztoka eneo hilo kuidhinishwa haraka iwezekanavyo ili ziuzwe nje, ambayo itaondoa kizuizi cha biashara kilichowekwa mwaka 2009.

Kuzuiwa huko kuliwekwa na Kimberly Process (KP), shirika la kimataifa linalosimamia almasi, kufuatia ripoti za mauaji ya watu chungu nzima na udhalilishaji unaofanywa na majeshi ya usalama ya Zimbabwe katika eneo la machimbo la almasi huko Marange.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.