6 Septemba, 2010 - Imetolewa 04:33 GMT

Rais Kagame kuapishwa kwa muhula wa pili

Rais Paul Kagame

Baadhi ya marais wa nchi za kiafrika wamewasili nchini Rwanda kwa sherehe za kumuapisha upya rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

Kagame anaapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili ofisini baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi wa saba.

Aidha Kagame alichaguliwa tena kwa asilimia tisini na tatu ya kura zilizopigwa mwezi jana ingawa anaapishwa huku nchi yake ikikabiliwa na shutuma za jeshi kuhusika na mauaji ya halaiki ya watu katika nchi jirani ya Congo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa upinzani walizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo wengi wakiseama ni hali ya mbaya ya kisiasa iliyochochea kususia kwao. wamedai kuwa rais Kagama anawakandamiza kisiasa.

bbc.co.uk navigation

BBC © 2012

Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.