|
Nigeria wawika dhidi ya Uhispania
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Chipukizi wa Nigeria wamedhihirisha kwamba wakwao hutunzwa baada ya kuitandika Uhispania mabao matatu kwa moja na kuingia
fainali za kombe la dunia kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.
Nigeria wataonana na Uswisi ambao hapo awali waliitandika Colombia mabao manne kwa bila. Fainali ni Jumapili 15 Novemba kwenye mji mkuu Abuja. Wenyeji walionekana wakakamavu tangu mwanzo huku wakishambulia kwa mizinga. Bahati yao ilisimama kabla ya kipindi cha mapumziko. Ingawa Wahispania walirejea na ari mpya huku wakimfanyisha kazi kipa wa Nigeria, vishindo vyao viliambukia patupu kila mara. Mabao ya Nigeria yalifungwa na Stanley Okoro na Sani Emmanuel Wahispania walipata kituliza jasho kupitia bao la Borja mnamo dakika ya 83. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||