|
Mchezaji Sudan kuchapwa kwa "unywaji"
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mchezaji nyota kutoka Nigeria, Stephen Worgu, anayesakata kabumbu nchini Sudan, amepatikana na hatia ya kunywa pombe, na amehukumiwa
adhabu ya kutandikwa bakora.
Worgu anachezea miamba ya Sudan, Al Merreikh, wenye ngome yao huko Omdurman kaskazini mwa nchi hiyo. Kilevi ni marufuku katika Sudan Kaskazini kunakokaliwa na idadi kubwa ya waislamu, ingawa inaruhusiwa Kusini ambako hakuna idadi kubwa ya waislamu. Adhabu kwa mshambuliaji huyo hodari bado haijatekelezwa, kwasababu mwanasheria wake amekata rufaa. Endapo rufaa yake itakataliwa, Worgu atanyukwa bakora 40 na kutakiwa kulipa pauni 250 za Sudan yapata dola za kimarekani 100. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||