BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 11 Novemba, 2009 - Imetolewa 15:32 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Harambee Stars wajifua bila kocha
 
Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, iko njia panda na itacheza mechi dhidi ya Nigeria bila kocha wake Antoine Hey, wakati itakapokuwa ikiwania fursa ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Kocha wao kutoka Ujerumani, Antoine Hey, hatasimamia timu hiyo katika mechi yao siku ya Jumamosi kufuzu kwa kombe la dunia 2010 dhidi ya Super Eagles.

Shirikisho la soka Kenya, Football Kenya Limited, (FKL), limesema kuwa Antoine Hey, amekuwa akikosekana katika mazoezi ya timu hiyo kwa kipindi cha siku tatu.

Harambee Stars wanatakiwa kuifunga Nigeria mjini Nairobi siku ya Jumamosi na watumai kuwa Msumbiji watachapwa na Tunisia, ili waweze kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika 2010.

Hata hivyo, Super Eagles bado wana uwezeokano wa kupata tiketi ya kwenda Afrika Kusini kwenye kombe la dunia.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha