BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 07 Novemba, 2009 - Imetolewa 19:46 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Pata uhondo wa Ligi Kuu ya Uingereza
 
Wolverhampton 1 Arsenal 4

Mwenye nguvu mpishe! Huenda ndiyo adhabu Wolverhampton walibaki nayo nyumbani baada ya kucharazwa mabao manne kwa moja na Arsenal. Kwa kipindi kirefu Arsenal walidhibiti mtiririko wa mechi huku wakizusha zogo kwenye lango la Wolverhampton kiasi cha kuwatunukia Arsenal mabao mawili ya kwanza! Kisirani kiliwaangukia Ronald Zubar na mwenzake Jody Craddock. Baadaye Arsenal walijaza yao wenyewe kupitia Cesc Fabregas na Andrey Arshavin.

Aston Villa 5 Bolton 1

Hatimaye Aston Villa wameanza kulenga shabaha ya kuona lango. Wamehakikisha matano yamemiminika kwenye wavu dhidi ya Bolton ambao walijaribu kujiondolea aibu kwa kujibu kwa bao moja.

Blackburn 3 Portsmouth 1
Jason Roberts alifunga mabao mawili kuipa Blackburn Rovers ushindi dhidi ya Portsmouth ambao wanaendelea kuvuta mkia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Portsmouth walikuwa wamejitosa uwanjani kwa mikiki na kufunga bao la kwanza kufuatia zinga la Jamie O'Hara.

Manchester City 3 Burnley 3
Kasi na magoli kemkem ndiyo hali ilivyokuwa kati ya Manchester City na Burnley. Hii ilikuwa mara ya tano mfululizo kwa Manchester City kutoka sare na kwa Burnley, ilikuwa mara ya kwanza kunyakua angalau pointi moja kutoka kwa mechi yao ya ugenini.

Tottenham 2 Sunderland 0
Ushindi wakati fulani hukiuka ufundi. Sunderland walionyesha ujuzi wa hali ya juu huku wakigongagonga lango la Tottenham bila mafanikio. Lakini Tottenham walikuwa wajanja. Walinyakua nafasi zao za magoli na kuiadhibu vikali Sunderland.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha