|
Afisa afukuzwa kazi juu ya Semenya
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Afisa mmoja mkuu wa riadha nchini Afrika kusini ameachishwa kazi kwa muda kuhusiana na namna alivyoshughulikia kashfa kuhusu
jinsia ya mwanariadha Caster Semenya.
Taarifa kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini humo SASCOC inasema Leonard Chuene ambaye ni mkuu wa shirikisho la riadha nchini humo pamoja na wanachama wake wote watachukuliwa hatua za kinidhamu. Bwana Chuene amekiri kudanganya kuhusu ikiwa ni kweli Semenya alifanyiwa uchunguzi kubaini jinsia yake. Hata hivyo afisa huyo alikataa kujiuzulu. Shirikisho la riadha Afrika Kusini lilitoa taarifa ya kuomba radhi kutoka kwa Semenya, familia yake, Rais pamoja na wananchi wote wa Afrika Kusini kwa namna swala la jinsia ya Semenya lilivyoshughulikiwa. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||