|
|
 |
 |
Elimu
Familia na Wanawake Katika makala hizi huwa tunakuwa na mfululizo wa vipindi maalum vya mafunzo. Vipindi ambavyo tumewahi kuvitangaza kwa Huko nyuma tumewahi kutangaza vipindi vinavyohusiana na Maisha ya familia ikiwa ni pamoja na kuzaliwa kwa mtoto hadi kuzeeka na kufa kwa kiongozi wa familia na Matatizo na mafanikio ya wanawake wa Kiafrika.
UKIMWI, Mihadarati na Wazee Vipindi hivyo vilifuatiwa na makala za Maradhi ya UKIMWI na jinsi yanavyoathiri maisha ya watu na uchumi wa nchi; Athari za Madawa ya Kulevya kwa taifa na hasa vijana; Matatizo na maendeleo ya walemavu; Maisha ya Wazee na harakati zao za kujikwamua kiuchumi.
Watoto, Mapenzi na Haki Mafanikio ya makala hayo ya elimu yalitupa moyo kuongeza mfulululizo wa vipindi vya Athari za vita kwa watoto waishio kwenye maeneo yenye migogoro; Ukiukaji na utekelezaji wa Haki za Mtoto kulingana na Mkataba wa kimataifa; Masuala ya uhamiaji yanayowahusu waafrika waliopo Ulaya; Maisha ya Mapenzi kulingana na mila na desturi za Kiafrika na pia maingiliano ya utamaduni wa kigeni; na Utekelezaji wa Haki za Binadamu kulingana na Mkataba wa Kimataifa.
Maelezo zaidi ya vipindi Ikiwa utapenda maelezo zaidi au kanda za makala hizo zilizopita wasiliana nasi kwa njia ya email: swahili@bbc.co.uk. Kama unataka maelezo zaidi kuhusiana na vipindi vyetu vya Dunia ya Watoto, Maisha ya Mapenzi na Haki za Binadamu soma katika ukurasa huu.
(Tunaomba radhi kwa kuwa ukurasa huu upo chini ya matengenezo. Tunashukuru kwa uvumilivu wako)
Vijana Leo na Jifunze Kiingereza Vipindi hivi vya elimu vinapokezana na makala ya Vijana Leo kila Jumamosi 1530GMT na Jumapili 0300GMT, 0400GMT na 1615GMT; Vile vile tuna makala za Jifunze Kiingereza kila Jumamosi na Jumapili 1745GMT. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na vipindi vya Kiingereza kwa wanaozungumza Kiswahili, soma katika ukurasa huu: English learning and teaching
|
|
 |
 |
|
|
 |
 |
 |
 |
 |
 |
 |
|
|
| BBC haina dhamana juu ya yale yaliyoandikwa katika kurasa za internet za mashirika mengine |
 |
| Wasiliana Nasi |
 |
| Email:swahili@bbc.co.uk |
 |
Au tuandikie Bush House, Strand, London WC2B 4PH |
Tel: + 44 207 557 2502 Fax: + 44 207 240 4637
|
|