A Guide to Swahili - 10 facts about the Swahili language in Swahili

Useful facts about the Swahili language in Swahili. © BBC - Jeff Overs
Translation in English

English version


Download buttonDownload mp3 - right click and choose 'save target as'

Open/close
1. Kiswahili kinazungumzwa wapi?

Kiswahili ni lugha ya taifa Tanzania na Kenya, na pia kinazungumzwa Uganda, DRC na visiwa vya Komoro. IPia kinazungumzwa kidogo Burundi, Rwanda, Kaskazini mwa Zambia, Malawi na Msumbiji.

Neno Kiswahili linatoka kwenye lugha yenyewe. Jina lake linatokana na wingi Sawahil kutoka kwenye neon la lugha ya kiarabu Sahil, ambalo maana yake ni mipaka au pwani. Ki- kwenye mwanzo wa neno, Kiswahili inamaanisha lugha ya pwani.

Open/close
2. Unachojua kuhusu Kiswahili

Mbali na Kiarabu, Kiswahili kimekopa baadhi ya maneno yake kutoka lugha ya Kiingereza, kwa mfano:

polisi, police
boksi, box
hoteli, hotel
televisheni, television
baiskeli, bicycle
hospitali, hospital
soksi, socks
picha, picture
muziki, music
redio, radio

Pia kuna maneno kama safari ambalo kwa Kiingereza inamaanisha kuvumbua kitu au nchi kwa kusafari, kuwinda wanyama mbugani, kama mbuga za wanyama Afrika na pia zilizopo bara la Australia. Neno chai kwa Kiingereza ni chai pia.

Open/close
3. Ugumu wa kujifunza?

Kiswahili ni lugha rahisi barani Afrika kujifunza kwa anayezungumza Kiingereza.Ni moja kati ya baadhi ya lugha ambazo haina sauti za mianguko na mipandisho kama Kiingereza. Pia ni rahisi kukisoma kwasababu maneno yanasomwa kama yalivyoandikwa.

Mtu anayezungumza Kiarabu, anaweza kujifunza kwa urahisi kwa sababu Kiswahili kinaambatanisha maneno ya lugha ya Kiarabu na sehemu za Kibantu Afrika Mashariki.

Moja katika ya tofauti na Kiingereza ni kwamba Kiswahili kina viambatanishi mwanzoni wa neno kuashiria majira ya tukio/tendo (kwa wakti huu ama wakati uliopita) na watu (mimi, wewe, nyinyi, wao).

Mathalan: Kutoka kwenye tendo kwenda go, I am going maana yake ninakwenda. Ni inaashiria I na na inaashiria nafsi. Viashiria vya utangulizi wa kutamka:

Ni, I - umoja
A, he/she/it - umoja
Wa, they - wingi
Tu, we/us - wingi

Baada ya viashiria vya mwanzo wa sentensi inaongezwa kuashiria kitenzi cha tukio/tendo

Na, kwa wakati uliopo
Li, kwa wakati uliopita
Ta, Kwa wakati ujao
Me, kwa wakati wa sasa

Kwa hiyo, ali-kwenda: he/she/it went, wata-kwenda: they will go, tume-kwenda: we have gone.

Open/close
4. Maneno ya kuzungusha ulimi

Wale wari wa Liwale wala wali wa Liwali

Mjomba mjomba kamchapa mkia wa komba

Kichwa cha twiga

Mpishi mbishi kapika mchicha mbichi

Kipi kikusikitishacho?
Kikusikitishacho ni moja ya maneno marefu katika lugha ya Kiswahili. Si neno linalosimama peke yake, lakini unapujumisha na neno kipi inaleta maana ya What's bugging you?, Unasumbuliwa na nini?

Open/close
5. Utani kwa Swahili

Mtoto alitumwa gazeti la tarehe nane (8), akaenda kwa muuza magazeti kununua gazeti lakini alipofika alikuta gazeti la tarehe nane hakuna kwa hiyo akachukua magazeti ya tarehe nne (4) mawili.

Open/close
6. Nikijifunza Kiswahili, kitanisaidia na lugha nyingine?

Asilimia 35 ya manenkatika lugha ya Kiswahili inatokana na maneno ya Kiarabu. Hii ni kutokana na zaidi ya karne 12 ya uhusiano na waliozungumza Kiarabau na watu wa pwani ya kisiwa cha Zanzibar. Kiswahili pia kimepata maneno kutoka kwenye lugha kama Persian, Kiingereza, Kireno, Kijerumani na Kifaransa na uhusiano toka karne tano zilizopita.

Kiswahili kinakua lugha ya kuzungumza ama lugha mama ya Afrika Mashariki na Kati ambayo ni sababu nzuri ya kujifunza.

Open/close
7. Cha kusema na kutokusema

Neno ambalo linaweza kuchanganya inategemea utakavyolitamka ni barabara; inaweza kumaanisha barabara (road) lakini ukilegeza ulimi na kukazia kwenye kwenye herufi 'r' inamaanisha kuafiki.

Kuna maneno ambayo yana maana tofauti kama maziwa. Linaweza kumaanisha maziwa (milk) lakini kuna wanaozungumza Kiswahili wanatumia hilo kumaanisha matiti (breast). Neno linalotumiwa sana ni matiti.

Open/close
8. Misemo yanayojulikana na methali

Hakuna Matata ni msemo maarufu na umepata umaarufu wake kwenye filamu ya katuni The Lion King.

Methali za Kiswahili zina maana nyingine, tofauti na maneno yanayoandikwa. Sana zinatumika kwenye mashairi ya wanamuziki. Mfano wa methali:

Dalili ya mvua ni mawingu
Maana: Unaweza kuona mafanikio kwa ishara.

Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.
Maana: Kila kizuri kina madhara yake.

Haraka haraka haina Baraka.

Maana:Ukifanya jambo kwa pupa mara nyingi linaharibika.

Wapiganapo tembo wawili ziumiazo nyasi.
Maana: Matajiri hasa wa kibiashara wanaposhindana, masikini ndio wanaopata tabu.

Open/close
9. Kumbukumbu na machapisho ya zamani za kale

Barua zilizoandikwa mwaka 1711, kisiwani Kilwa, ndio zinaaminika kuwa ndio nyaraka za kwanza kuandikwa kwa Kiswahili. Barua hizo zilitumwa kwa Wareno walioshi Msumbiji na zimehifadhiwa kwenye makumbusho ya Historia za Maktaba ya Goa nchini India.

Nyaraka za kale za mwaka 1728 zinaonyesha shairi linaloitwa Utendi wa Tambuka ambalo limeandikwa kwa Kiswahili kutumia maandishi ya Kiarabu. Kutokana na kushawishika na utawala na kikoloni kutoka nchi za Ulaya, maandishi ya Kilatini ndio yanayotumika kuandika lugha ya Kiswahili.

Open/close
10. Namna ya kuwa na heshima

Ukitaka kuuliza swali, anza na neno kwa. Mfano: kwa hisani yako naomba kikombe cha chai? au Tafadhali naomba uninunulie gazeti.

Ukimkanyaga mtu kwa bila kukusudia unaweza kusema kumradhi au samahani. Jibu rasmi ni samahani haigombi.

Ukikutana na mtu kwa mara ya kwanza, anza kwa kumsalimia na kusema habari. Kutegemea na muda wa siku, unaweza kusema habari za asubuhi, habari za mchana au habari za jioni.

Sio vizuri kumuita mtu kwa kutumia neno wewe kwa hiyo muite mtu kwa jina lake au cheo ama wadhifa wake mfano: baba au mama ama Mheshimiwa.

UNESCO World Heritage site, Stone Town, Zanzibar, Tanzania. © BBC - Jeff Overs

Facts about Swahili

10 things to know about the Swahili language

Residents of Stone Town in Zanzibar. © BBC/Jeff Overs

Swahili key phrases

Get started with 20 audio phrases

© BBC - Jeff Overs

The Swahili alphabet

Learn the letters of the Swahili alphabet

BBC © 2014 The BBC is not responsible for the content of external sites. Read more.

This page is best viewed in an up-to-date web browser with style sheets (CSS) enabled. While you will be able to view the content of this page in your current browser, you will not be able to get the full visual experience. Please consider upgrading your browser software or enabling style sheets (CSS) if you are able to do so.