« Iliyopita | Mwanzo | Inayofuata »

Kuna hisia kuogopwa timu za Hispania

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-12-10, 14:32

Hatimaye timu 16 zitakazocheza hatua ya mtoano kwa michuano ya kuwania Ubingwa wa Ulaya kwa vilabu imekamilika na timu zimejulikana. Kinachosubiriwa ni kupangwa nani atakumbana na nani katika hekaheka hizo. Kumejitokeza suala la baadhi ya timu kufanya bidii na kumaliza wakiwa wa kwanza katika makundi yao, eti kuzikimbia ama Barcelona au Real Madrid. Watalaamu wa soka wanasema, unapotaka kuwa bora kwa soka basi ujiandae kukabiliana na kuzitoa timu zilizo bora. Hakuna haja kuogopana wakati huu kwani  Barcelona na Real Madrid ni wanadamu kama wengine, timu zijiandae tu kuwavaa uwanjani. Au unasemaje mpenzi wa soka?

Maoni Weka maoni

  • 1. Muda 8:54 siku 2010-12-11, Faith aliandika:

    Suala linalojitokeza hapa si kuogopa kukutana na El Classico au the Catalans ila kadri michuano inavyo canja mbuga ndivyo timu zinavyoimarika na kuibuka na mbinu bora zaidi za kiufundi. Hivyo, vilabu vinafahamu kwamba haviwezi kuwa bingwa bila kukutana na hao vinara wa Spain lkn havipendi suala hili lijiri katika hatua za awali. Kama unavyofahamu Ndg. Charles Hilary kwamba kadri unavyosonga mbele katika micuano hii hususan katika hatua za mtoano ndivyo unapopata alama (Credit) za ubora katika viwango vya soka na hata kuvutia wadhamini na wawekezaji wengine ambao wamekuwa muhimu sana katika zama hizi za soka lenye ushindani mkubwa.

    Kwa hivyo ni suala la muda tu, sidhani kama hawa wahispaniola wanaogopwa kiasi hicho. Na kwa kumalizia soka kwa sasa ni mbinu na si jina la klabu mfano mzuri tunauona kwa El Classico walipoadhiriwa Nou Camp na the Catalans. Au Arsenal walipopoteza mechi zao mbili dhidi ya Shakhtar Donesk na Bragha na kulazimika kushinda mechi yao ya mwisho didi ya vibonde Partizan Belgrade ili kujihakikishia nafasi katika 16 Bora.

  • 2. Muda 11:58 siku 2011-01-14, Fulgence Lendo aliandika:

    Mi nadhani hao wanaohusika na uteuzi wanashindwa kutekelezamajukumu yao kikamilifu.haiwezekani timu mbili tu ndo zenye wachezaji wenye viwango duniani.au labda huwa hawaangalii ligi nyingine duniani?hapo wamechemsha.

Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

Copyright © 2015 BBC. Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.