« Iliyopita | Mwanzo | Inayofuata »

Tevez asaidiwe arudie hali yake

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-11-06, 13:52

CARLOS TEVEZ  amekuwa katika hali ngumu kujikwamua na matatizo yanayosumbua akili yake kiasi cha kushindwa kucheza soka kwa kiwango chake cha kawaida.

Nahodha huyo wa Manchester City amefanya ziara za siri mara tatu kumuona daktari baada ya kuruhusiwa kurejea Argentina kuiangalia familia yake.

Tevez, mwenye umri wa miaka 26, analipwa paundi za Uingereza 150,000 kwa wiki, lakini anakabiliana na matatizo ya kuwa na homa ya nyumbani kiasi cha kumfanya asifikirie kusakata kandanda tena kwa vile hawezi kuwa mbali na watoto wake  Florencia, mwenye umri wa miaka mitano na Katie aliye na umri wa miezi minane.

Mfungaji mabao maarufu wa Manchester City, Tevez ametengana na mkewe Vanesa, sasa anazuzuliwa na msichana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni muigizaji wa Kiagentina, Brenda Asnicar, 19, ambaye amemwambia Tevez akirejea England hataambatana nae.

Tevez inavyoonekana hilo linamsumbua sana, jee asaidiwe vipi mshambuliaji huyu wa Argentina na timu ya Manchester City?
Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

Copyright © 2015 BBC. Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.