« Iliyopita | Mwanzo | Inayofuata »

Pele na Maradona nani zaidi?

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-10-25, 10:28

Hivi karibuni mchawi wa soka duniani Pele alitimiza umri wa miaka 70 akiwa bado mwenye nguvu na afya njema. Alisifika enzi zake kwa uwezo wake mkubwa wa upigaji chenga, kutoa vyumba safi kwa wafungaji wenzake, kufunga kwa vichwa mithili ya mpira uliopigwa kwa mguu na alikuwa na nguvu ya miguu. Huyo ni pele aliyeanza kuichezea timu ya taifa ya Brazil katika Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 1958.

Msakata kandanda mwengine hodari kuwahi kutokea duniani ni Diego Maradona anayefikisha umri wa miaka 50. Akiichezea timu yake ya taifa ya Argentina alikuwa chachu ya ushindi kwa kikosi kikali cha nchi hiyo katika Kombe la Dunia. Hivi sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Argentina, ambapo alishindwa kuipelekea Kombe la Dunia nchi yake wakati wa mashindano ya Afrika Kusini mwaka 2010.

Wapenzi wa soka duniani kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka kumaliza ubishi kati ya wanasoka hawa wawili bora zaidi duniani, nani alikuwa zaidi ya mwenzake?

Fifa iliwahi kuchapisha kura ya kumtafuta mchezaji bora wa soka wa karne, lakini hawakufurahishwa baada ya matokeo kuonesha Maradona  ndiye aliyeshinda.

Kwako mpenzi wa soka uliye mkereketwa hata kama hukuwahi kuwashuhudia wakisakata soka enzi zao, unadhani kati ya wawili hawa, Pele na Maradona nani alikuwa zaidi? Ni mjadala wa siku nyingi lakini si vibaya tukiuamsha upya wakati wachawi hawa wa soka wakiwa wnasherehekea siku zao za kuzaliwa.

Maoni Weka maoni

  • 1. Muda 12:50 siku 2010-11-16, range simon aliandika:

    habari za jioni watangaza wa bbc.nafikiri pele ni bora kuliko maradona kutoka ufungaji wa mabao na heshima yake.mbona hakuna utaratibo wowote wa kuchagua mchezaji bore wa afrika mwaka jana katika bbcswahili.com

  • 2. Muda 16:44 siku 2011-01-21, julias aliandika:

    NAWAPONGEZA WATANGAZJI WA BBC KWAKUTULETEA MATANGAZO YA MPIRA YA LIGI KUU YA UINGEREZA

Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

Copyright © 2015 BBC. Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.