« Iliyopita | Mwanzo | Inayofuata »

Afrika Kusini yataka kuwa mwenyeji wa Olimpiki

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-13, 18:14

Kabla vumbi la michuano ya Kombe la Dunia halijatulia, Afrika Kusini inajitokeza tena kwa mara nyingine kujaribu kuweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuandaa michezo ya Olimpiki.

Hayo yamebainika baada ya nchi hiyo kuthibitisha kuwa inaandaa mipango ya kuwasilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa michezo ya 2020.

 

 

socc.jpgWaratibu wanatumai kwamba mafanikio ya mashindano ya Kombe la Dunia yaliyokamilika tarehe 11 Julai, yatatoa nafasi ya kukubalika kwa urahisi kuipeleka michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Afrika.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki bado haijaanza mchakato huo, lakini mwenyeji wa michezo hiyo atajulikana katikati ya mwaka 2013.

Miji mingine iliyoonyesha ni ya kuwania ni Budapest wa Hungary, Busan wa Korea Kusini, wenyeji wa Michezo ya Jumuiya ya Madola - Delhi ya India, vile vile Taiwan, Dubai na Italia zinatarajiwa kujitosa pia.

Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

Copyright © 2015 BBC. Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.