Kumbukumbu za 2010-07

Raul wa Madrid ataka kuhamia England

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-27, 19:28

Maoni (0)

Wengi mtamkumbuka Raúl González Blanco, au Raul, enzi akiwa mshambuliaji hatari wa Real Madrid, lakinii sasa ametangaza kutaka kuiacha timu hiyo kubwa ya Hispania.

 

Soma taarifa hii kwa kirefu

Brazil yapata kocha mpya, ni Mano Menezes

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-23, 18:28

Maoni (0)

Kocha Mano Menezes wa timu ya klabu ya nyumbani, Corinthians, sasa ndiye kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Brazil.


Soma taarifa hii kwa kirefu

Ufaransa yafungia wachezaji wote wa Kombe la Dunia

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-23, 15:41

Maoni (1)

Shirikisho la Soka la Ufaransa, FFF, katika hatua ya kipekee limewafungia mechi moja wachezaji wote 23 wa timu ya taifa waliocheza Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Hatua hiyo ni kujibu mapigo, baada ya matatizo ya nidhamu kuathiri ufanisi wa timu hiyo ambayo ilitolewa katika hatua ya kwanza.

Wachezaji wa waligoma kufanya mazoezi baada ya mwenzao, mshambuliaji Nicolas Anelka kutimuliwa kutokana na kumtukana kocha Raymond Domenech.

Arsenal wanamfukuzia Mesut Ozil kutoka Werder Bremen

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-22, 12:18

Maoni (1)

Arsene Wenger anajaribu kusuka kikosi maridadi kitakachomudu vishindo vya Ligi Kuu ya Soka ya England, baada ya kuambulia patupu kwa misimu kadhaa, mojawapo ya shabaha zake ni kumnasa Mesut Ozil kutoka Werder Bremen ya Ujerumani.

Soma taarifa hii kwa kirefu

Chelsea kumkosa Czech kwa mwezi mmoja

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-22, 10:32

Maoni (0)

Mabingwa watetezi wa England, Chelsea watamkosa mlinda mlango Petr Czech kwa mwezi mmoja, ni baada ya kujeruhiwa akiwa mazoezini.

Soma taarifa hii kwa kirefu

Vuvuzela itadumu Afrika, hata kama Ulaya inapingwa

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-21, 12:17

Maoni (1)

Vuvuzela ni kifaa kilichopata umaarufu na maadui vile vile. Kwa wanaofutilia mechi za soka za Afrika Kusini, hakuna tofauti, vuvuzela ni sehemu ya soka. 

 

vuvuz.jpgVuvuzela haikuanza jana au leo, ilipata umaarufu zaidi wakati wa mashindano ya CONFEDERATIONS, kisha KOMBE LA DUNIA kutokana na matangazo ya televisheni, redio na wavuti kuonekana na kusikika kote duniani. VUVUZELA ilikuwepo na itakuwepo, kwa mtizamo wangu. 

Lakini kwa wenzangu na mimi walioichukia, hii ni fursa kwao kusema hawataiki kuiona wala kuisikia katika viwanja vya vya soka.Wanasahau kuwa huo ni

Tumesikia vilabu vya ligi kuu ya soka ya England vikisema ni marufuku kuhangaika na vuvuzela, unapoingia kwenye viwanja vyao, potelea mbali unalipa tiketi au umeingia bure.

Tottenham, Arsenal, Everton na Birmingham, tayari wamebainisha chuki yao dhidi ya vuvuzela.

Wapige vita wasipige, mechi zitakazochezwa Afrika zitaendelea kupambwa na "nyuki" za vuvuzela.

Nini maoni yako? Unaunga mkono au unapinga? Sababu gani?

 

Steven Gerrard ajifunga kusalia Liverpool

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-21, 12:12

Maoni (1)

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, ameihakikishia timu yake kuwa ataendelea kubakia Anfield, msimu ujao.

Soma taarifa hii kwa kirefu

Joe Cole akimbilia Liverpool

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-19, 18:51

Maoni (0)

Joe Cole baada ya kuona atasugua mkeka kwenye timu ya Chelsea, amehamia Liverpool ambako ana matumaini ya kupata nafasi ya kucheza.

Kijana huyo aliyechezea timu ya Fabio Capello kwenye Kombe la Dunia, amesaini mkataba wa miaka minne.

Kocha Harry Redknapp alionyesha nia mapema, lakini Joe Cole alichelewa kuamua, ilipofika Jumatatu, akaamua kumwaga wino kuchezea Liverpool.

Capello kupata msaidizi "kijana mzawa"

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-16, 18:06

Maoni (0)

Meneja wa timu ya England, Fabio Capello, amekubali kuteua kocha kijana ambaye ni mzawa wa England ajumuike na Stuart Pearce kwenye kikosi chake cha ufundi, BBC Sport imefahamishwa.

Soma taarifa hii kwa kirefu

Afrika Kusini yataka kuwa mwenyeji wa Olimpiki

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-13, 18:14

Maoni (0)

Kabla vumbi la michuano ya Kombe la Dunia halijatulia, Afrika Kusini inajitokeza tena kwa mara nyingine kujaribu kuweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuandaa michezo ya Olimpiki.

Soma taarifa hii kwa kirefu

Kombe la Dunia: Wakosoaji wamefunga midomo

Hassan Mhelela Hassan Mhelela | 2010-07-12, 13:23

Maoni (3)

Wakosoaji wa Afrika Kusini kama mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia wamekosa cha kusema, kama utakumbuka, walipaza sauti kuibeza nchi hiyo ya kwanza barani Afrika kuwa haitaweza kuandaa shughuli hiyo kubwa.

 

100712112352_somali_kibonzo_600x400_nocredit.jpgLakini baada ya fainali ambayo Hispania ilitwaa taji kwa ushindi wa goli 1-0, kelele zote za kusema viwanja havitakuwa tayari, hoteli hazitatosha, uhalifu umekithiri zimetoweka - hata wasiotaka kuisifia Afrika Kusini wametafuta njia za kusema mashindano yamefanyika kwa utaratibu mzuri.

Kulikuwa na wasi wasi miongoni mwa nchi za Ulaya, ambako baadhi ya mashabiki walidai wanahofia usalama wao, kutokana na takwimu kuonyesha kuwa nchi hiyo ina matukio mengi mno ya mauaji kwa mwaka.

Waswahili wanasema adui yako muombee njaa, hapa tumeona nchi za Ulaya na kwingineko zilitaka kuiombea njaa, si Afrika Kusini pekee, lakini pia bara zima la Afrika.

Je, nchi za Afrika zinaweza vipi kutumia mfano huo wa Afrika Kusini kufanya mambo makubwa na yenye manufaa kwa wananchi wao?

Ingawa hoja inaweza kuibuka, je nchi za Afrika zimeambulia nini? Hilo tutaliweka kando, linahitaji mjadala tofauti.

Kombe la Dunia: Baadhi ya vituko vya waamuzi

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-07-02, 12:33

Maoni (0)

Mengi yamezungumzwa kuhusu makosa yanayofanywa na waamuzi katika mashindano ya Kombe la Dunia hapa Afrika Kusini, hapa naorodhesha baadhi tu, na wewe kama unakumbuka lolote, ruksa kupachika maoni yako.


1.Mshika kibendera wa Uruguay, Mauricio Espinosa aliyeshindwa kuona mpira ukivuka mstari kumnyima Frank Lampard bao katika mechi ya England na Ujerumani.
 
2.Koman Coulibaly kutoka Mali mechi ya Marekani na Slovenia aliyekataa bao wazi la Maurice Edu.
 
3.Brazil na Ivory Coast - mwamuzi kutoka Ufaransa, Stephane  Lannoy, aliyeruhusu bao la Luis Fabiano mchakato wake mpira akiwa ameugusa kwa mkono mara mbili kabla ya kufunga.
 
4.Argentina na Mexico, mwamuzi mzoefu Roberto Rosetti wa Italia aliyeruhusu bao la Carlos Tevez, lilionekana dhahiri mfungaji ameotea. Argentina ilishinda mabao 3 -1 dhidi ya Mexico.
 
5.Mwamuzi Wolfgang Stark wa Ujermani,  hakuweza kuona mchezaji wa Argentina akimzuia mchezaji wa Nigeria wakati Gabriel Heize alipofunga bao pekee.
 
6.Ujerumani na Serbia mwamuzi Alberto Undiano alitoa kadi nyekundu kwa mshambuliaji wa Ujerumani, Miroslav Klose kwa faulo ambayo wala haikuwepo. Hali iliyomsababishia Klose kukosa mchezo dhidi ya Ghana.
 
7.Mwamuzi kutoka Columbia, Oscar Ruiz, alimtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo wa Ufaransa, Yoann Gourcuff kwa kumchezea faulo MacBeth Sibaya wakati baadaye iliporudiwa katika TV haikuwa faulo ya kadi nyekundu.
 
8.Australia na Ujerumani, mshambuliaji wa Australia Tim Cahill alipata kadi ya kwanza nyekundu ya Kombe la Dunia kwa mashindano ya mwaka huu huku ikionekana si rafu ya kadi nyekundu. Mwamuzi kutoka Mexico, Marco Rodriguez ndiye aliyefanya kituko hicho.
 
9.Bao la kuotea la Shane Smeltz lilionekana kuwashtua wapenzi wa soka katika Kombe la Dunia, mshika kibendera hakuona mfungaji kama ameotea, ulikuwa mchezo baina ya New Zealand na Italia.
 
10. Chile na Hispania.Marco Rodriguez alitomtoa nje kwa kadi nyekundu Marco Estrada wa Chile kwa kumkwatua Fernando Torres. Ilipooneshwa kwenye TV ilionekana hakukusudia ni ajali tu ya kugongana wachezaji.
 
Je, kuna haja ya Sepp Blatter kuomba radhi kwa kila kosa lifanywalo na waamuzi? na hapo teknolojia ikukubaliwa kuendesha mpira, sijui itakuwaje pale itakaposema mpira umeingia wakati umegonga nyavu za nje!!

Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

Copyright © 2015 BBC. Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.