Michezoni homepage

Ligi ya England, jee Liverpool kuwemo nne bora?

Charles Hilary Charles Hilary | 2011-02-07, 12:56

Maoni (0)

Baada ya kumtimua Roy Hodgson na nafasi yake kuchukuliwa na Kenny Dalglish, Liverpool sasa inaanza kurejea katika eneo lake la msimamo wa Ligi kuu ya Soka ya England.

Alipochukua nafasi ya umeneja Kenny Dalglish, bado Liverpool ilikuwa haijazinduka kutoka usingizini, ila sasa ukungu wa kuona nyavu za wapinzani machoni mwa wachezaji umetoka na wanafunga katika karibu kila mechi, mfungaji wao mkuu akiwa Raul Meireles.

Hivi karibuni waliilaza Fulhma bao 1-0, baadae wakashukia Stoke kwa mabao 2-0 na mfupa mkubwa uliokuwa pengine ukiwatia hofu mashabiki wake, Chelsea, wakauweza baada ya kushinda ugenini bao 1-0.

Kinachoonekana ni Liverpool wanaelekea kurejea eneo lao la nne bora kwani kwa sasa wanashikilia nafasi ya sita ya msimamo wa ligi.

Jee kasi hii itadumu hadi mwishoni mwa Ligi, nionavyo mimi wanazidi kuimarika kila kukicha na hilo linawezekanha.

Tutarajie sura mpya Chelsea msimu ujao?

Charles Hilary Charles Hilary | 2011-01-25, 11:40

Maoni (0)

Wapo wanaosema nusu ya wachezaji wa Chelsea kwa sasa wana umri wa miaka 30 na kupindukia. Pengine ndio kigezo cha kushindwa mikiki mikiki ya vijana wa timu nyingine, katika kuutetea ubingwa wao msimu huu. Mimi sijui.

Lakini wiki hii kumekuwa na uvumi  kuna uwezekano Chelsea ya msimu ujao ikajaa vijana wengi kwa vile wakongwe wanatazamia kuihama klabu hiyo au kulazimishwa kuhama. Wametajwa akina Anelka, Drogba, Terry, Ashley Cole, Lampard, Benayoun, Paulo Ferreira, nikiwataja wachache tu, kwa vile umri wao ni miaka 30 na zaidi basi ni wakati wa kupisha damu changa.

Tumeona hivi karibuni Meneja Carlo Ancelotti, akiwapa nafasi angalao ya kipindi cha pili baadhi ya vijana walioonekana kumudu sawasawa vishindo vya Ligi Kuu ya England. Mshabiki mwenzangu wa soka utakubaliana nami mlinzi Jeffrey Bruma, Gael Kakuta, Josh McEachran na Daniel Sturridge, walipopewa nafasi wameonesha uwezo mkubwa na kuwa kioo cha siku zijazo kwa mafanikio ya Chelsea.

Pamoja na hayo jee ni vyema kuwapangua wakongwe wote hao wa Chelsea kwa mkupuo msimu ujao kwa lengo la kujenga timu imara yenye damu changa?

Dirisha dogo la usajili Ligi Kuu ya England

Charles Hilary Charles Hilary | 2011-01-19, 14:42

Maoni (0)

Hivi sasa vilabu mbalimbali vya ligi Kuu ya soka ya England, vimo katika harakati za kujiimarisha kwa awamu ya pili ya msimu, kwa kusajili wachezaji ambao wanadhani watawavusha wakiwa katika malengo waliyojiwekea.

Tottenham wameshamtia kibindoni, Steven Piennar aliyetoka Everton, Aston Villa nao wakiwa wanajitahidi wasishuke daraja, wameamua kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kumsajili Daren Bent kutoka Sunderlan.

Manchester City nao mbali ya kutumia pesa nyingi tangu msimu uliopita kusajili wachezaji imara, wanaona bado haitoshi, wamefanikiwa kumpata mfunga mabao hodari kutoka klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani, Dzeko, aliyekuwa mpachika mabao mahiri kwa ligi ya Bundesliga ya Ujerumani, hao ni kwa uchache. Kwa mtazamo wako wakati huu unadhani klabu uipendayo ingejiimarisha vipi katika kumalizia msimu vile ungependa?

Zaidi kutoka blogu hii...

bbc.co.uk navigation

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.