Kumbukumbu za 2010-12

Mdudu mbaya ang'ang'ania Chelsea, kuna nini?

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-12-28, 15:05

Maoni (1)

Walianza kwa kishindo wakiwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, timu za awali kukumbana nao, walizabwa mabao mengi tu, kuna timu ziliezekwa mabao hadi 6. Timu nyingine zikaingia hofu kwamba Chelsea bado wagumu na wamedhamiria kweli kutetea ubingwa wao.

Mambo yakaenda kubadilika, Chelsea ikaanza kuwa mkarimu wa mabao, wakiruhusu kufungwa hata nyumbani kwao. Mambo yakazidi kuwa magumu kila mechi.

Mashabiki wa soka na hasa wa Chelsea wanajiuliza kimewakuta nini "wakongwe" hao wa Chelsea?

Na jee tutarajie mabadiliko ya meneja Carlo Ancelotti, kama ilivyokuwa desturi ya mmiliki kubadilisha mameneja  timu inapofanya vibaya.

Hapana shaka yoyote kama alivyosema Ancelotti wanaweza kurudi katika mbio za kuutetea ubingwa wao, lakini si kwa aina ya mchezo wanaocheza.

Wewe mpenzi wa soka unayefuatilia Ligi Kuu ya Soka ya England, ungewapa mawazo gani ya kujikwamua na nyani huyu aliyewaganda mgongoni Chelsea?

Kuna hisia kuogopwa timu za Hispania

Charles Hilary Charles Hilary | 2010-12-10, 14:32

Maoni (2)

Hatimaye timu 16 zitakazocheza hatua ya mtoano kwa michuano ya kuwania Ubingwa wa Ulaya kwa vilabu imekamilika na timu zimejulikana. Kinachosubiriwa ni kupangwa nani atakumbana na nani katika hekaheka hizo. Kumejitokeza suala la baadhi ya timu kufanya bidii na kumaliza wakiwa wa kwanza katika makundi yao, eti kuzikimbia ama Barcelona au Real Madrid. Watalaamu wa soka wanasema, unapotaka kuwa bora kwa soka basi ujiandae kukabiliana na kuzitoa timu zilizo bora. Hakuna haja kuogopana wakati huu kwani  Barcelona na Real Madrid ni wanadamu kama wengine, timu zijiandae tu kuwavaa uwanjani. Au unasemaje mpenzi wa soka?

Zaidi kutoka blogu hii...

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.